Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi ya Viongozi, kubeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja leo.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif na baadhi ya viongozi wakiwa katika dua ya kumuombea aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Unguja, marehemu Mussa Hamis Silima, aliyefariki,Agosti 23 katika hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam, alikolazwa baada ya kupata ajali Agosti 22. Marehemu Silima amezikwa leo katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja.
Rais wa Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakiwa katika shughuli ya mazikonya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Silima. Maziko hayo yamefanyika leo katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja
Rais wa Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakiwa katika shughuli ya maziko hayo.
Waziri Mstaafu, Edward Lowassa, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima.
|
Sehemu ya Kinamama waliojitokeza katika shughuli hiyo ya maziko.
Wakazi wa Kijiji cha Kiboje na vitongoji vyake wakijumuika katika shughuli ya maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja leo.
No comments:
Post a Comment