Habari za Punde

*WAREMBO WA VODACOM MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA TARANGIRE

 Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Tarangire, mkoani Manyara jana walipokwenda kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo ya tano kwa ukubwa nchini. 
Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani kwa watanzania. 
Katika hatua nyingine leo Miss Photogenic anataraji kutangwazwa na kujipatia tiketi ya kuingia katika nusu fainali ya shindano la Vodacom Miss Tanzania, ambapo Miss Photogenic atakuwa ni mrembo wa pili kuingia katika hatua hiyo ya 15 bora baada ya Top Model. Picha na Father Kidevu Blog
 Mshiriki wa Vodacom Miss Tanzania Zelulia Manoko, akizungumza kwa niaba ya wenzake baada ya kufika katika lango kuu la kuingilia hifadhi ya taifa ya Tarangire mkoani Manyara jana na kujionea wanyama wa aina mbalimbali.   
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiingia katika lango Kuu la hifadhi ya taifa ya Tarangire mkoani Manyara jana walipofika kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo ambayo ni ya tano kwa ukubwa nchini. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.