Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba katika ufunguzi wa mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF), uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF) anayemaliza muda wake Balozi Sten Rylander, wakiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha leo, wakati Makamu wa Rais, alipofika kufungua mkutano wa 20 wa Magavana wa Afrika (ACBF).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa 20 wa Magavana wa Afrika, baada ya kufungua mkutano hu.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF), uliofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, katika Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha leo.
No comments:
Post a Comment