Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MDAHALO WA KATIBA KUHUSU UMUHIMU WA KATIBA KATIKA MAISHA YA WATANZANIA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania, uliofunguliwa leo, katika Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Joseph Butiku (wa pili kushoto) wakati akiiwasili kwenye Jumba la Makumbusho ya Taifa leo kwa ajili ya kufungua Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika maonyesho ya Jumba la Makumbusho ya Taifa kuangalia picha za baadhi ya Mashujaa wa Harakati za ukombozi zilizowekwa katika jumba hilo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim na (kulia) ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Joseph Butiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma moja ya kitabu kilochokuwa katika meza ya maonyesho ya vitabu katika Jumba la Makumbusho ya Taifa, baada ya kufungua rasmi Mdahalo wa wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania, uliofunguliwa leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa katika mdahalo huo kutoka Unguja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi wa Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim (kushoto) na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati) wakiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA) Willbroad Slaa, nje ya ukumbi, wakati Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania, uliofunguliwa leo, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.