Mwandishi wetu
BENDI ya muziki wa dansi ya African
Stars “Twanga Pepeta International” itafanya onyesho kwa mara ya pili nchini
Uingereza Jumamosi hii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,
Mkurugenzi wa kampuni ya Afrikan Stars Enterteinment (ASET), Asha Baraka
alisema kuwa jumla ya wasanii 13 wanatarajiwa kwenda huko kwa ajili ya
kusherehekea miaka 50 ya Uhuru na Watanzania wahishio huko.
Baraka alisema, wanamuziki wao
wanatarajiwa kuondoka Ijumaa na shoo itafanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa
Silver Spoon, Wembley bendi hiyo ikiwa huko itaendelea kufanya shoo zake kama
kawaida nchini.
Mara ya kwanza kwa bendi hiyo kufanya
shoo ilikuwa mwaka 2007 ambapo ilifanya shoo kwa wiki tatu katika miji
mbali mbali mikubwa duniani.
Alisema, mgeni rasmi katika shoo hiyo
anatarajiwa kuwa Balozi wa Tanzania wa Uingereza ambaye ni Peter Kallaghe na
maandalizi yanaendelea vizuri ya safari hiyo.
“Kama unavyofahamika kuwa Tanzania
tulitawaliwa na Waingereza na huko wapo Watanzania wanaohishi huko tumeona ni
vyema tukaenda kuungana nao wenzetu kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya
Uhuru, alisema Baraka.
“Wasanii wanaoenda huko ni 13 na wengine
watabaki kuendelea na shoo kama kawaida kwenye kumbi mbalimbali kwenye viwanja
vya Leaders tutaungana na Msondo Ngom,” alisema Baraka.
No comments:
Post a Comment