Habari za Punde

*ZIARA YA MO KATIKA MRADI WA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA UNAOFADHILIWA NA BADEA SINGIDA MJINI.

  Mo Dewji, akiongozana na viongozi wasimamizi wa mradi wa ujenzi na kupata maelezo ya sehemu mbalimbali ndani ya eneo la Ujenzi la mradi wa Tanki kubwa na la kisasa kutoka kwa mmoja wa wataalum wa kampuni ya Spencon Service Ltd alipotembelea mradi huo eneo la Mandewa jana.
  Mkurugenzi wa SUWASA, Injinia Isaack Nyalonji, akitoa maelezo ya kisima kikubwa cha mradi wa BADEA katika eneo la Mwankoko, kushoto kwake Mbunge Mo Dewji alipotembelea kukagua mradi huo ambao unatarajia kumalizika Julai mwakani. Wa pili kushoto, Mstahiki Meya, Shehe Salum Mahami, eneo la chanzo cha mradi huo wa maji.
  Moja ya Tanki la maji ambalo litakua likipokea maji na kusambaza sehemu nyingine mbalimbali. Mradi huu unajengwa na wataalamu kutoka kampuni ya Spencon Service Ltd.
Mo Dewji akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa mradi huo wa BADEA ambao unatarajiwa kumalizika Julai mwakani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.