Habari za Punde

*HALI NI MBAYA DAR YOTE HALI NI TETE YAJAA MAJI MADARAJA YABOMOKA MENGINE HAYAPITIKI, WATU KADHAA WALIPOTIWA KUFA

Haya ni baadhi tu kati ya maeneo yaliyojaa maji yatokanayo na mvua kubwa inayoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam, hapa ni maeneo ya kati ya Tabata na Buguruni, kama picha hii inavyoonyesha nyumba zikiwa zimefunikwa na kuelea majini leo hii.Eneo hili ni sehemu unapopita Mto Msimbazi ambao umeharibu madaraja kadhaa yanayounganisha eneo moja na jingine.
Eneo la Tabata unapopita Mto Msimbazi likiwa limejaa maji na kufunika baadhi ya nyumba za maeneo hayo leo.
Haya ni maeneo ya Vingunguti kuelekea Tabata, eneo la Viwanda.
 Hapa ni katika Daraja la Kawe eneo la Bondeni linapojengwa Daraja jipya tayari pakiwa pameshazuiliwa kupita kutokana na daraja hilo kuweka nyufa za kukatika kwa daraja hilo ambalo maji yamelizidia na kupita juu.
 Kingo za Daraja hilo zikiwa tayari zimebomoka kutokana na kuzidiwa nguvu na maji hayo ya mvua kubwa iliyonyesha leo.
 Baadhi ya abiria wakitembea kwa miguu baada ya eneo hilo njia kufungwa na kuzuiliwa kutopita magari baada ya maji kujaa na kupita juu ya Daraja.
 Uwanja wa Ndege pia katika Maegesho ya Ndege ndogo asubuhi ya leo ulikuwa umejaa maji, lakini ndege ziliweza kuendelea na safari zake kama kawaida.
Mto Msimbazi ulikopita na kuharibu Miundombinu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.