Mussa Hussein akiwa katika Ufukwe kabla ya kuanza safari yake ya kuelekea 'Nungwi'
* ASHAURI ABIRIA KUFAHAMISHWA MBINU ZA KUJIOKOA
MUSSA HUSSEIN: Kitu ambacho kitakuwa tofauti na show nyingine ambazo mimi nimewahi kufanya ni kwamba hapa nitakupa stori za ajali za kuzama kwa meli sio ya Nungwi pekee bali hata zilizopita nikikuonyesha matukio yenyewe yalivyokuwa tofauti na unaposoma kwenye gazeti au kusikia redioni.
Kwa mfano katika taarifa ya habari utaonyeshwa kwa sekunde 30 tu mchezo umekwisha.
Hivyo huwezi kugundua haya matukio ni makubwa au ni madogo kiasi gani
MO BLOG: Nini kimekufanya ufikie maamuzi ya kufanya kipindi cha namna hii kinachoonyesha matukio halisi au huridhishwi na jinsi taarifa za majanga zinavyotolewa?
Kwa sababu kila siku anayeandika anasema Ajali za Barabarani zitatumaliza, Ajali za angani zitatumaliza, Ajali za majini zitatumaliza kila siku ni hivyo hivyo. Na ukiangalia hizi ajali za sijui meli, treni, mabasi zinaua mamia ya watu.
No comments:
Post a Comment