Habari za Punde

*VODACOM YAWASHUKURU WATEJA WAKE KWA KUWACHANGI WAATHIRIKA WA MAFURIKO, TAYARI ZIMEPATIKANA SH. M.6.2

  Vodacom Tanzania inawashukuru wote ambao tayari wameshaonyesha moyo wa upendo na mshikamano wao kupitia kampeni ya ‘Red Alert’ na kufanikisha kukusanya jumla ya Sh.milioni  6,284,000/= kati ya December 22, 2011 hadi December 27, 2011, kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waloathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
“Tunapenda kutoa wito kwa wananchi ili waendelee kuchangia Ndugu zetu waliopatwa na janga la mafuriko kwani bado wanahitaji misaada yetu,kwa Kupitia nambari ya Red Alert 15599 mteja anaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi–SMS yenye neno MAAFA na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.
Jinsi ya kuchangia kwa m-pesa
*150*00# kupata orodha ya huduma za m-pesa.
Hatua ya 2: Chagua 4 – Lipa Bili
Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni – weka namba 155990
Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu – weka namba yako ya simu
Hatua ya 5: Weka kiasi – ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea
Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri
Hatua ya 7: Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.