Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AOMBOLEZA KIFO CHA ALIYEKUWA MBUNGE NA NAIBU WAZIRI WA FEDHA, JEREMIA SUMARI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa. Sumari anatarajia kuzikwa kwao Arumeru siku ya jumatatu baada ya kuagwa rasmi siku ya Jumamosi nyumbani kwake Mbezi Beach.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mke wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, Mama Miriam Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu jijini Dar es Salaam leo.
  Makamu wa Rais, Dkt Bilal, akisalimiana na Spika wa Bunge, alipowasili nyumbani kwa marehemu Sumari. Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na watoto wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari.
Katibu Mkuu wa CCM, Mukama, akiweka saini katika kitabu hicho cha maombolezo.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.