Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jioni hii ametuma saram za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa, Kamanda Mkuu wa Polisi ndugu na Jamaa wa askari wawili waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Mombo wakati msafara wa Makamu ukitokea Lushoto kuelekea Tanga baada ya kumaliza ziara yake katika Wilaya hiyo ya Lushoto leo jioni.
Gari hilo la askari lililokuwa mwisho wa msafara liliacha njia katika kona ya mwisho ya kutokea Lushoto kuingia Mombo na kusababisha vifo vya askari wawili pamoja na majeruhi. "Ndugu zangu naungana nanyi kutoa salamu hizi za pole za mheshimiwa Makamu wa Rais kufuatia ajali iliyotokea leo".

No comments:
Post a Comment