Habari za Punde

*NAHODHA WA MELI YA CONSTA CONCORDIA ILIYOPINDUKA AENDELEA KULAUMIWA

  IDADI  ya watu wasiojulikana walipo baada ya meli ya kifahari ya Consta Concordia, kupinduka katika eneo la  Italia Ijumaa iliyopita, imefikia watu 29, watu sita kati yao wakiwa wamethibitishwa kufariki.
Wakati shughuli za uwokozi zikiendelea, shirika la habari la Italia (Ansa), limeripoti kuwa Nahodha wa meli hiyo, Francesco Schettino, amelaumiwa kwa kukwepa juhudi za kuwaokoa waliokuwa wakizama katika meli hiyo.
Nahodha huyo ambaye hivi sasa anaendelea kuhojiwa na maofisa wa polisi, pia amelaumiwa na mwenye meli kwa kuacha makusudi kufuata njia ya kawaida ya meli hiyo, jambo lililosababisha kutokea kwa ajali hiyo.
Hata hivyo Nahodha huyo anasisitiza kuwa alifuata utaratibu sawa wakati wote alipokuwa katika meli hiyo.
Hihi sasa Nahodha huyo amekamatwa  kwa tuhuma za mauaji, na leo hii Jaji anatarajiwa kutoa maamuzi na kuamua iwapo nahodha huyo mweye umri wa miaka 52 ataendelea kushikiliwa na polisi ama la.
Italia imesema itatangaza hali ya tahadhari kufuatia kupinduka kwa meli hilo, na kwamba itatoa msaada kuzuia janga lolote kwa mazingira.
Waziri wa mazingira wa Italia anasema anahofia kuwa mafuta huenda yakavuja kutoka kwenye meli hiyo na kusababisha uchafuzi wa mazingira.

Watu ambao bado hawajapatikana ni pamoja na wafanyikazi wa meli hiyo pamoja na abiria kutoka Marekani, Ufaransa na Italia.








No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.