Habari za Punde

*SHEREHE YA HARUSI YA MKWERE WA MIZENGWE WAGENI WAALIKWA WAVUNJIKA MBAVU NI VITUKO MWANZO MWISHO

  KATIKA sherehe ya harusi ya msanii mahiri wa maigizo ya Vichekesho nchini wa kundi la Mizengwe, Hemedi Maliyaga, mahiri na maarufu kwa jina la ‘Mkwere’ ilikuwa ni aina yake kutokana na aina na staili ya uendeshwaji wa sherehe hiyo iliyotawaliwa na vimbwanga vya kila aina.
Chereko, vifijo, shangwe, nderemo na vigelegele vilitawala kila kona ya ukumbi huo huku wageni waalikwa wakivunjika mbavu kutokana na vituko vilivyotawala  ukumbini humo kuanzia wasimamizi wa Maharusi hadi wanakamati.
Sherehe hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Delux Sinza, jijini Dar es Salaam  usiku wa Ijumaa iliyopita, ilimvutia kila aliyehudhuria ukubini hapo kiasi cha wengine kushindwa kusimama kwenda katika foleni ya kuchukua chakula muda ulipofika wakijisikia kuendelea kucheka tu hali yak u kuwa mchekeshaji ndo kwanza akiendelea na mambo yake.
Mkwere, amefunga ndoa na Bi. Fatma Abdallah, ambapo baadhi ya watu walisikika wakisema ukumbini humo, “Duh! Ama kweli jasiri haachi asili, Sijui kama huyu Bi harusi hataugua kwa kuchekeshwa na mumewe ndani ya nyumba maana kila afanyalo huyu Bwana ni la kuvunja mbavu” alisema mmoja wa wageni waalikwa ukumbini humo. Picha kwa hisani ya UNIQUEENTERTZ
Mmoja kati ya wasanii wa kundi la Mizengwe, Oha, akisakara Bolingo kwa staili ya kipekee ukumbini hapo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.