Habari za Punde

*KUFA KWA MUZIKI WA BONGO KUNACHANGIWA NA BAADHI YA WASANII WAKUBWA WA HAPA NCHINI

 Tulitegemea kwa wasanii wakubwa kama Ambwene yesaya ama A.Y kama anavyofaamika kwa mashabiki wengi wa muziki, angekuwa ni mfano wa kuigwa na wanamuziki chipukizi hapa nchini, ila  baadala yake ameonekana kuwa kikwazo kikubwa cha kukua kwa muziki wa reggae na ragga hapa nchini.

Sisi kama Jahson na susu hatuwezi kujifunza lolote kutoka kwa msanii huyo (A.Y).
 
Wengi tunamjua A.Y kama msanii wa hip hop lakini mwaka 2010 aliwahi kushindania tuzo ya mwanamuziki bora wa reggae na hatimaye kupata tuzo hiyo na kuichukua kwa mbwebwe zote na Pia mwaka huu 2012 ameingizwa tena katika Category ya ragga na nina imani atapata ttena.

Anaweza kuibuka tena na tuzo hiyo kutokana ma madhaifu yaliyopo kwa waandaaji wa tuzo hizo za Kilimanjaro music award.

Bushoke alikuwa mfano mzuri sana wa kuigwa alipopewa tuzo ambayo hakustahili na kuikataa je A.Y kwa nini alikubali tunzo hiyo?

Na ki ukweli haikumstahili kwani wasanii kama A.Y wanatuvunja moyo sana sisi wasanii tunaofanya muziki huo pamoja na mashabiki wa muziki huo wa reggae na ragga na kwa taarifa yake tu bwana AY asijidanganye kwa wingi ama uchache wa kura hizo anazopata katika kinyang’anyilo hicho.

Na pia asidhani kama anapigiwa na mashabiki wa Reggae na ragga,no huo ni uongo mtupu ni mashabiki wake wa hip hop ndo wanaomuwezesha so anawakanganya wapenzi wake kiukweli.

Sisi kama washikadau wakubwa wa muziki huu wa Ragga na Reggae tumesikitishwa sana kwa mapungufu makubwa ya msanii huyo AY kuzidi kukumbatia ujinga unaofanyika kila mwaka sijui anataka tujifunze nini msanii huyo bwana Ay.

Atumchukii AY hapana ila tunajaribu kuweka mambo wazi na kutoruhusu ujinga huu kuendelea maana kunawakati ataimba Taarabu na na Bolingo na watamuweka kwenye category hiyo na atachukuwa tuzo.

Pia inawezekana kabisa akawa anauwa muziki wake ama anawagawanya mashabiki wake kwa kutotulia kwenye style ya muziki wake, na kuwa kama Inzi anavyotua mara kwenye embe bovu mara kwenye kidonda mara jalalani, atumuelewi bwana A.Y

Tungependa washikadau wa wakubwa wa muziki huu walione kama hili ni tatizo na walikemee kwa nguvu zote ili Tanzania iwe na ukomavu wa muziki huu tofauti na hapo tutakuwa tunapiga kwata bila kusonga mbele.

Sisi tumeshafanya nyimbo kama Heat na Show me some love ambazo zimefanya vyema katika vituo mbalimbali vya redio na Televisheni, lakini tumeenguliwa kwenye tuzo hizo hii inakatisha tamaaaa sana.

Lakini sisi hatutokata tamaa na wala haitufundishi uwoga wa kupingana na kitu ambacho tunaamini tunakifanya vvema kabisa japo kuna wasanii wengi wakali waliamua kuachana na muziki kwa ajiri ya mambo ya kinyama kama haya

Shabiki wetu jaribu kuingia kwenye youtube na usearch Jahson & Susu ama Jahson Tanzania alafu utoe coment je tunastahili kunyimwa tuzo hizo? Asanteni ni sisi Jahson na Susu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.