Habari za Punde

*MCHEZO WA YANGA NA MTIBWA SUGAR WAINGIZA SH. MIL 49/-


Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga ya Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Morogoro,  lililochezwa Februari 8 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 49,510,000.

Jumla ya watazamaji 14,604 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 112 kwa kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000 kwa VIP A.

Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 7,552,372.88 kila timu ilipata sh. 8,933,048.14, uwanja sh. 2,977,682.71.

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,191,073.08, TFF sh. 2,977,682.71, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,488,841.36, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 297,768.27 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni 2,977,682.71.

Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000.

Posho ya kujikimu kwa kamishna na waamuzi sh. 160,000, mwamuzi wa akiba sh. 30,000, tiketi sh. 4,000,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.

Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 1,022,280 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 876,280.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.