Habari za Punde

*MELI YA ITALIA BADO INAELEA KATIKA BAHARI YA HINDI

Mabaharia wa meli ya Costa Allegra iliyo na zaidi ya abiria 1000, walituma ujumbe wa kuomba msaada baada ya moto kuzuka na kuteketeza mitambo ya kuzalisha umeme, ikiwa takriban Kilomita 300 kusini mwa Ushelisheli.                    
 
Chombo kimoja cha uvuvi kutoka Ufaransa tayari kimewasili katika eneo hilo na maafisa wa Italia wamesema meli nyingine na mashua zinatarajiwa kuwasili katika eneo hilo baadaye adhuhuri ya leo kwa ajili ya kutoa msaada.
Kamanda Cosimo Nicastro kutoka jeshi la wanamaji la Italia ndiye anayesimamia shughuli nzima ya uokoaji huo.

Cosimo alisema kuwa mashua ya uvuvi iliyowasili katika eneo hilo inawasaidia  kuwasiliana na mabaharia katika meli  ya Costa Allegra.

Aidha kamanda Cosimo Nicastro, amesema hakuna mipango ya kuwaondoa abiria katika meli hiyo.

Meli hii inamilikiwa na kampuni ambayo ilishutumiwa vikali baada ya kutokea kwa ajali ya meli nyingine iliozama katika pwani ya Italia na kusababisha vifo kadhaa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.