Habari za Punde

*SAAD GADDAFI AITISHIA NYAU LIBYA, AAHIDI KURUDI KURIVENJI

Libya imelalamika kwa Niger, juu ya matamshi ya mtoto wa kiume wa Muammar Gaddafi ambaye sasa anaishi uhamishoni nchini Niger.

Akihojiwa na televisheni moja ya Kiarabu, Saadi Gaddafi alitishia kuongoza vita dhidi ya serikali ya Libya.

Ambapo alisema kuwa mapigano kadha yatazuka punde nchini Libya, na kwamba karibu kila siku anawasiliana na makundi yanayojiandaa na mapigano hayo yaliyomo ndani ya nchi hiyo.

Bwana Gaddafi, ambaye alikimbilia Niger baada ya serikali ya baba yake kupinduliwa Agosti mwaka jana, alisema anataraji kurudi Libya punde siku wala muda ambao hautawekwa bayana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.