Dkt. Ellen Otaru Okoedian, akitoa mwongozo kwa wawakilishi wa mabaraza ya Wanafunzi kutoka wilaya za jiji la Dar es Salaam wakati Shirika la Save the Children lilipofanya uzinduzi wa taarifa ya Lishe leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanafunzi wakiandika mapendekezo yao kwenye moja ya Bango kubwa maalum la EVERYONE, wakati wa uzinduzi huo leo.
Mh. Lediana N'gong'o na Bi. Hoyce Temu wakiainisha baadhi ya mambo muhimu yanayotakiwa kutekelezwa ili kufanikisha kampeni ya kupambana na utapiamlo hapa nchini.
****************************************
*MDAU WA HAKI ZA WATOTO HOYCE TEMU ASHAURI ELIMU YA LISHE ITOLEWE KWA WANANCHI.
Shirika la Save the Children Tanzania limesema licha ya kuwepo maendeleo, watoto wanne kati ya kumi wenye umri wa miaka isiyozidi mitano nchini Tanzania wamedumaa.
Katika muhtasari wa wa hali ya Tanzania inaonyesha asilimia 17 wameathirika sana na kila siku watoto 130 wanakufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na utapiamlo.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa lengo la Milenia namba 4 linalotaka kupunguza theluthi mbili ya vifo vya watoto haliwezi kufikiwa bila kukabiliana na utapiamlo.
Akizungumza wakati wa hafla ya chakula baada ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mh. Lediana Ng’ong’o ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya lishe ameshauri serikali kuajiri wataalam wa lishe ikiwezekana katika kila wilaya nchini.
Naye Mdau wa Kuhamasisha Haki za Watoto na Afya zao Hoyce Temu aliyealikwa katika uzinduzi huo, amesema ni muhimu serikali ikatoa elimu ya lishe kwa wananchi, ili waweze kutambua umuhimu wa kula chakula bora na faida zake kimwili na kiakili.
No comments:
Post a Comment