Habari za Punde

*SOKO LISILO RASMI KATIKA STENDI YA UBUNGO MATAA LAENDELEA KWA KASI YA AJABU, WAHUSIKA MNALIONA??

Wafanyabiashara wadogo wadogo wajulikanao kama wamachinga wakiwa wamepanga bidhaa zao katika kituo kidogo cha mabasi Ubungo kama picha hii inavyoonyesha.
 
Kwasasa biashara katika eneo hilo imeshamili na kuzidi kukua kila kukicha kiasi kwamba wahusika wamejisahau na kuona ni jambo la kawaida.
 
Pamoja na Serikali kuwajengea soko maalum ili waweze kufanya biashara zao katika mahala panapotambulika lakini bado wafanyabiashara hawa wamezidi kuvamia maeneo ya pembezoni mwa barabara na kupanga bidhaa zao kiasi cha kusababisha usumbufu kwa waenda kwa miguu wanaopita maeneo haya. Picha na Henry Henry
Wafanyabiashara wengine walikuwa wanafanya minada.
Kila kitu kinapatikana mahala hapa, hakuna haja ya kwenda sokoni ama madukani.

 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.