Wachezaji wa Yanga wakuelekeza mashambulizi langoni mwa Zamaleck, wakati wa mchezo huo wa Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo timu hizo zimetoka sare kwa kufungana bao 1-1.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Khamis Kiiza, ndiye aliyeanza kutikisha nyavu za Zamaleck ktika dakika ya 36, huku Zamaleck wakichomoa bao hilo katika dakika ya 74 kipindi cha pili kupitia mchezaji wake Amri Zakhi na kufanya Yanga kuwa katika wakati mgumu kufuzu hatua ijayo ya michuano ya Kombe la Washindi Barani Afrika na hasa ukizingatia mchezo wa marudiano utapigwa nchini Misri.
Mshambuliaji wa Yanga Khamis Kiiza, akishangia bao lake alilofunga katika kipindi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment