Habari za Punde

*YANGA YAICHAPA MTIBWA SUGAR 3-1 NA KUKAA KILELENI

MABINGWA watetezi wa Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara Yanga ya Dar es Salaam, wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, katika mchezo wa Ligi Kuu uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo sasa Yanga inaongoza Ligi hiyo huku ikiwa na Pointi 34 sawa na Mahasimu wao wa jadi Simba, ambapo inaongoza kwa kutumia kanuni za mchezo wa Soka kutokana na mahasimu hao kuwa na tofauti ya magoli.

Matokeo hayo ya leo yaliyoipaisha Yanga na kukaa kileleni yametokana na pointi 34 baada ya kucheza jumla ya mechi 16, huku mahasimu wao wa jadi, Simba nao wakiwa na mechi 16 mkononi walizocheza, ambapo Yanga inajumla ya mabao 28 ya kufungana ya kufungwa 13 huku Simba ikiwa na mabao 25 ya kufunga, na 10 ya kufungwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.