Habari za Punde

*BONDIA WA KIKE PENDO NJAU MAMA WA WATOTO WAWILI AFUNGUKA ZAIDI KUHUSU MAISHA YAKE

Bondia wa Kike, mkali wa mchezo wa Kick Boxer, Pendo Njau akipozi kwa picha na watoto wake wawili, mtoto wa kwanza Sabrina Lazaro (kushoto) na wapili Joseph Lazaro (mkononi).
*****************************************
*Aamua kuimarisha familia yake
*Afunguka zaid kuhusu maisha yake ya kifamilia

BAADA mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, kuripoti kuhusu Mwanadada mahiri katika mchezo wa ngumi na Kick Boxing, Pendo Njau kupata mtoto, wadau wengi wamekuwa na mawazo tofauti huku wakitaka kujua zaidi kuhusu maisha ya kifamilia ya mdada huyu.

Hivyo Mtandao huu ulizungumza na Mkali huyo na kuweka ahadi ya kuonana na kuzungumza ana kwa ana, na kuweza kujua mengi yaliyokuwa nyuma ya pazia.

Ilikuwa ni mida ya saa moja jioni wakati Sufianimafoto alipoweka ahadi ya kukutana na Pendo Njau na kutinga mitaa ya Mwananyamala Komakoma pande anazoishi Mdada huyo mkali na kufanya mazungumzo yaliyochukua kama dakika 20, hivi.

Baada ya kukutana na kuanza mazungumzo Pendo aliamua kuanza kufunguka zaidi pale alipoulizwa swali kuhusu Baba wa mtoto.

''Unajua wabongo bwana ni noma sana, wanajua sana kuzusha, kupanga na kufuatilia mambo ya watu, mimi nimesikia tu nikiambiwa baada ya watu kuona stori yangu katika Mtandao wako wa Sufianimafoto na gazeti la Nipashe, na wengine wakihoji mtoto ni wa nani mara hivi mara vile.

Mama wa mtoto ni mimi na Baba wa mtoto yupo Arusha na kwa taarifa yao huyu si mtoto wangu wa kwanza bali ni wapi, kwani mwanangu wa kwanza ni wa kike na hivi sasa ana umri wa miaka (5) anaitwa sabrina Lazaro na huyu wa ni wapi wa kiume anaitwa Joseph Lazaro, hivyo wasidhani ni kitu kipya kwangu kuwa na mtoto'', alisema Pendo

Aidha Pendo alisema kuwa pamoja na kuwa watoto wawili lakini bado haimsumbui katika kujiweka fiti kutokana na kwamba hatua hiyo ni hatua muhimua ambayo kila binadamu aliyekamilika hupitia ili kujenga familia ambayo ni urithi wa baadaye.

''Unajua Mume wangu wala haishi hapa jijini, anaishi Jijini Arusha kwa hiyo huwa mimi naenda tu na kurudi na mara nyingine huwa akija yeye, kwani kama unavyojua familia ni jambo la msingi sana katika maisha ya mwanadamu''. alisema Pendo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.