Habari za Punde

*LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA YAINGIA RAUNDI YA 21

LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara sasa inaingia raundi ya 21 ambapo kesho (Machi 14) kutakuwa na mechi mbili katika ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga ya Dar es Salaam ambao watakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuikabili African Lyon.
Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni ni sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 15,000.
Mechi nyingine ya kesho itachezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambapo Simba watakuwa wageni wa timu ya Polisi Dodoma.
Yanga itarejea tena uwanjani Machi 17 mwaka huu kwa pambano dhidi ya wenyeji Villa Squad litakalofanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati siku hiyo hiyo Coastal Union itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
Machi 18 mwaka huu kutakuwa na mechi tatu ambapo Simba itakuwa ugenini Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar, Toto African itaikaribisha Polisi Dodoma jijini Mwanza wakati Azam na Ruvu Shooting Stars zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Chamazi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.