Habari za Punde

*MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA HARAMBEE YA CHANGIA ELIMU KATA YA KIPAWA (W) ILALA

 Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (alievaa trakisuti ya Blue) akikata utepe kuzindua Matembezi ya Mkakati wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu katika Kata ya Kipawa, Manispaa ya Ilala, mkoa wa Dar es Salaam leo.(pichani kutoka kulia wapili mwenye miwani) ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala.Jerry Slaa,(akifuatiwa na alievaa trakisuti nyeupe) Diwani wa Kata ya Kipawa Bona Kalua, hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na wadau wa sekta ya uboreshaji wa Miundombinu ya elimu na mazingira wa kata hiyo, Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete, akiongoza matembezi ya Uzinduzi wa Mkakati wa Uboreshaji wa Muindombinu ya Elimu katika Kata ya Kipawa, Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni maalum kwa ajili ya kuanza harambee ya kuchangia huduma za elimu katika Kata hiyo. Mpango huo umebuniwa na Diwani wa Kata hiyo, baada ya kuona hali halisi katika shule moja yenye wanafunzi zaidi ya 2000 iliyopo Katika Kata  hiyo ikiwa na Choo kimoja tu kinachotumiwa na Walimu na Wanafunzi kwa zamu zamu na madarasa machache katika shule hiyo ya Kata. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.