Mshambuliaji wa Man U, Wayne Rooney, akishangilia moja ya bao lake aliloifungia timu yake katika mchezo wa leo jioni dhidi ya West Brom Albion uliochezwa katika Uwanja wa Old Trafford, ambapo Man U imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kufikisha jumla ya Pointi 67 ikiwa na tofauti ya pointi 1 tu na Man City wenye Pointi 66, wakifuatiwa na Tottenham wenye pointi 53. Mabao ya Man U, yalifungwa na Wayne Rooney dakika ya 35 na 71, huku bao la kwanza akipewa pande safi na Javier Hernandez na la pili pasi ya Ashley Young. Mpaka sasa United imeshacheza jumla ya mechi 28.
Mwamuzi wamchezo kati ya Man U na Bromwich Albion's, Lee Probert, akimuonyeka kadi nyekundu mchezaji wa Bromwich, Jonas Olsson, wakati wa mchezo huo.
Beki wa Swansea, Ashley Williams (kulia) akijiandaa kuchukua mpira baada ya mshambuliaji wa Man City, Sergio Aguero , kuanguka, wakati wa mchezo huo, ambapo mpira huo baada ya kutoka hapa ndipo lilipatikana bao la ushindi kwa timu hiyo.
Mfungaji pekee wa bao moja na la ushindi katika mchezo kati ya Man City na Swansea, (kulia) akichuana kuwania mpira na beki wa Man City.
Mshambuliaji wa Man City, Mario Balotel, akiwa hoi bila kuamini kilichotokea uwanjani hapo baada ya mchezo kumalizika huku timu yake ikibamizwa bao 1-0.
No comments:
Post a Comment