Habari za Punde

*NAPE NNAUYE ASAKA NAMBA JUKWAA LA TWANGA, AMUACHA HOI ASHA BARAKA KWA KUIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYOTE

 Hapa Nape akipiga gitaa la Solo. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,  Nape Nnauye, jana alipata fursa ya kipekee kujiunga na Bendi ya Twanga Pepeta "Kisima Cha Buruduni" na kufanya nao mazoezi ndani ya ofisi za Aset zilizopo Kinondoni.

Baada ya kufanya makamuzi ya nguvu ilidhihirika wazi kwamba ukiachilia mbali siasa Nape ni msanii mkali wa kuimba, na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki.

Aidha Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka alifurahishwa na kumshukuru sana Nape kuja kuwatembelea na kuwapa sapoti, vilevile alimuahidi kuwa nafasi yake itakua wazi kwenye bendi mara tu atakapo amua
kuachia ngazi kutoka katika jukwaa la siasa na kuamua kujiunga katika tasnia ya muziki.
 Nape, akizichapa Tumba katikati ya Sebene.
 Nape akicharaza Gitaa la Besi..
 Nape, akikaanga 'Chips' yaani akizichapa Drams, ''Hiki kipaji we acha tu''....
Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka, akifurahia mambo makubwa aliyokuwa akifanya Nape ukumbini hapo wakati wa mazezi ya bendi hiyo. Picha Zote na Frank Eyembe

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.