Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA jana jioni kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku tatu mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama. PICHA NA IKULU
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Moshi jana jioni kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.
Miongoni mwa shughuli ambazo Mheshimiwa Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up
Shughuli hiyo itakayofanyika leo Jumatatu, asubuhi, imepangwa kuanzia katika Lango la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)
.
Mbali na kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.
Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea Mkoa huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment