Mkurugenzi wa mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Serena Dar es salaam leo wakati alipotangaza udhamini wa kampuni hiyo katika maadhimisho ya wiki ya maji yanayotarajiwa kufanyika mkoani Iringa kuanzia Machi 16.Kulia ni Nandi Mwiyombela Maeneja wa Mahusiano (SBL) na katikati Amani Mafuru Naibu Mkurugenzi wa maji Vijijini.
******************************
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
ZAIDI ya watu 500, 000 wanatarajiwa kunufaika baada ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SLB) kutenga zaidi ya sh.milioni 300 kwa ajili ya miradi salama ya maji na usafi kwenye mikoa minne nchini .
Hayo yalisemwa leo(jana) na Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano kwa kampuni hiyo, Teddy Mapunda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya maji yatakayofanyika kitaifa mkoani Iringa kuanzia Machi 16 hadi 22,mwaka huu.
Alisema kati ya fedha hizo sh. milioni mbili zitatumika katika miradi ya maji kwenye mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Dares Salaam na Iringa. Aliongeza kuwa katika mkoa wa Iringa fedha hizo zitatumika kuzindua mradi wa uvunaji wa maji na uboreshaji wa miundombinu maeneo ya hospitali, wakati sh. milioni moja kudhamini vipeperushi na vijarida.
“Tunawekeza fedha hizo mahali ambapo tuna viwanda kwa sababu tukitumia maji inabidi tuyarudishe,” alisema Teddy.
Teddy alifafanua kuwa SBL inafanya kazi kupunguza matumizi ya maji katika vifaa vya uzalishaji na mfululizo wa toaji wa bidhaa zao, ambapo inahusisha uboreshaji madhubuti wa maji katika mitambo yao, kuhakikisha matumizi ya maji katika maeneo yanazingatiwa na kupunguza majitaka.
Aliongeza kuwa wamekusuia kuongeza njia za upatikanaji wa maji kwenye jamii zinayowazunguka na usimamizi wa vyanzo vya maji.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maji Vijijini, Amani Mafuru alisema maadhimisho hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Samora, hivyo aliwataka wannachui wajitokeze ili kuweza kushiriki , kutoa tathimini na kuishauri serikali kuhusu sekta hiyo.
Tatizo la maji limekuwa likiathiri kila bara duniani na zaidi ya asilimia 40 ya watu.
Hadi kufikia mwaka 2025 watu bilioni 1.8 watakuwa wanaishi katika ama mikoa ambayo haina majisafi kabisa , na theluthi mbili ya idadi ya watu duniani inawezekana wanaishi katika hali ngumu ya upatikanaji wa maji.
No comments:
Post a Comment