Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI NA KUZINDUA RIPOTI YA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, zilizofanyika leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Katika sherehe hizo pia Makamu wa Rais alizindua Ripoti ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria Tanzania Bara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe, kuzindua Ripoti ya Mafanikio ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria kwa upande wa Tanzania Bara, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Malaria Duniani zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda (wapili kushoto) ni Kaimu mkuu wa Wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala, Jordan Lugwimbana.
 Mmoja kati ya viongozi wa mradi huo wa Malaria akizungumza.
 Baadhi ya waliotunukiwa Tuzo ya Ripoti ya Mafanikio ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria, wakifurahia na kuinuka juu baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi, Makamu wa Rais.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Barnaba, akiimba jukwaani na watoto wa shule za msingi wakati wa sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.