Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars.
Mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) na Zimbabwe iliyokuwa ichezwe keshokutwa siku ya Jumamosi (Aprili 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam imefutwa.
Uamuzi huo umefanywa na Chama cha Mpira wa Miguu Zimbabwe (ZIFA) ambayo sasa imeamua kucheza mechi ya kirafiki na Zambia, ambayo itachezwa Aprili 28 mwaka huu jijini Harare, siku ambayo ilikuwa imepangwa kupigwa mchezo huo hapa nyumbani.
Twiga Stars inaendelea na mazoezi chini ya kocha wake Charles Boniface Mkwasa, katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) iliyoko Ruvu mkoani Pwani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea na jitihada za kuitafutia mechi za kirafiki Twiga Stars kabla ya kucheza mechi ya mashindano dhidi ya Ethiopia ambayo itafanyika Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa.
No comments:
Post a Comment