Habari za Punde

*SHUGHULI ZA MAZIKO YA WAKILI THEONEST RUTASHOBORWA MKOANI KAGERA

 Picha ya marehemu Theonest Rutashoborwa, ukiwa mbele ya Jeneza lenye mwili wake wakati wa shughuli za maziko yake yaliyofanyika katika Kijiji cha Bukabuye Mkoani Kagera jumatano ya wiki iliyopita. Theonest alikuwa ni Mjumbe wa Kamati tendaji ya Klabu ya Yanga.
 Jamali Malinzi (kulia) Criss na baadhi ya washirika wa karibu wa marehemu wakiwa eneo la tukkio na waombolezaji wengine katika msiba huo.
 Waombolezaji wakiomboleza kwa masikitiko makubwa kuondokewa na kipenzi chao.
 Kipukuso akiwa ni mmoja kati ya waombolezaji, mahala hapo.
 Mamaa wa Yanga, (wa pili kushoto) akijumuika na waombolezaji wengine kijijini hapo.
 Mama wa Marehemu, Theresa akiwa na majonzi...
 Jamali Malinzi, akitoa nasaha na maneno ya Shukrani baada ya maziko.
Mshirika wa karibu wa marehemu, Theonest, Wence Mtui, ambaye ndiye aliyeratibu safari ya washirika hao kutoka jijini Dar es Salaam hadi Kagera kwa ndege ya kukodi, akitoa maneno ya shukrani, baada ya maziko. Mtui amewashukuru wale wote wadau wa karibu na marehemu, ndugu, Jamaa na Marafiki walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli hiyo ya maziko. 
Wadau, kutoka (kushoto) Wence Mtui, Benny Kataruga na Jastus, wakiwa uwanja wa ndege wa Kagera tayari kurejea jijini Dar es Salaam, baada ya kumaliza shughuli za maziko hayo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.