Habari za Punde

*WACHEZAJI 9 WA POLISI DODOMA WALIMWA FAINI YA SH. MILIONI 1 KILA MMOJA

KAMATI ya Ligi ya TFF imewafungia mechi tatu na kuwapiga faini ya sh. milioni mmoja kila mmoja wachezaji tisa wa timu ya Polisi Dodoma baada ya kumpiga mwamuzi Martin Saanya kwenye mechi dhidi ya Azam iliyochezwa Aprili 14 mwaka huu mjini Dodoma.
 
Wachezaji hao walioadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 25(g)(iii) ni Noel Msekwa, Frank Sindato, Abdallah Matila, Bantu Admin, Salmin Kisi, Madope Mwingira, Sihaba Mkude, Kaliyasa Mashaka na Ibrahim Massawe.
 
Iwapo wachezaji hao watahama Polisi na kujiunga na timu nyingine, watahama na adhabu zao.
 

Vilevile timu ya Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri. Pia timu hiyo imepewa barua ya onyo kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi dhidi yao na Yanga iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.