Habari za Punde

*WADAU WA MICHEZO WAFAIDI UHONDO WA HEINEKEN CHAMPIONS PLANET

 Wana habari, Majuto Omary (kushoto) na Millard Ayo wakiwa katika picha ya pamoja na warembo Hamissa Hassan mshiriki wa Miss Tanzania mwaka jana na marafiki zake kabla ya kuanza kushuhudia Live mechi kati ya Bayern Munich na Real Madrid.
 Meneja Mkuu wa Heineken, Rodney Hensen akiwa na Michael Mbungu na warembo wa Heineken wakati wa uzinduzi wa nyumba ya Heineken Champions Planet iliyopo Masaki jijini.
Mtaalam wa masuala ya media wa kampuni ya Push Mobile, Juila Jessie akiwa pamoja na mchekeshaji maarufu, Evans Bukuku wakibadilishana mawazo katika nyumba ya burudani na michezo ya Heineken Champions Planet iliyopo Masaki jijini.
Picha zote kwa hisani ya kampuni ya Push Media Mobile.
*******************************
Na Mwandishi wetu
Wadau mbali mbali wa michezo nchini jana walifaidi uhondo wa nyumba mpya ya kuangalia mechi za igi ya Mabingwa Ulaya ijulikanayo kwa jina la Heineken Champions Planet iliyopo maeneo ya Masaki jijini.
Wadau hao walishuhudia timu ya Bayern Munich ikiirarua timu ngumu ya Real Madrid kwa jumla ya mabao 2-1 na kujiwekea mazingira mazuri ya kucheza fainali ya mwaka huu ya mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.