Habari za Punde

*ZILIZOPATIKANA KUHUSU KIFO CHA KANUMBA KUAGWA LEADERS JUMANNE

 Mmoja kati ya wasanii akibebwa na waombolezaji baada ya kuzimia nyumbani kwa Kanumba wakati wa maombolezo hayo.


Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Kanumba Sinza, leo wakiomboleza kifo cha msanii Steven Kanumba.


 HABARI za awali ambazo kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Afande Kenyela,  zilisema kuwa, Kanumba, kabla ta kifo chake kulitokea hali ya kutoelewana Mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la Lulu, ambaye pia ni msanii wa Filamu, huku habari cha vyanzo zikitonya kuwa, wapenzi hao waligombana na Kanumba kusukumwa na kuanguka kisha kugonga kichwa chini na kupoteza fahamu.

Aidha watonyaji waliendelea kusema kuwa Kanumba, akiwa bafuni home kwake wakati akioga, ghafla alimsikia mpenzi wake huyo akichonga na njemba nyingine kwa simu na ndipo alipotoka na kuhoji kuwa huku akihitaji simu ya mpenziwe ili kumjua huyo aliyekuwa akichonga na mpenziwe kwa wakati huo tena akiwa home kwake.

 
Alipohitaji simu ya mpenziwe ndipo ulipozuka ugomvi na huku baadhi ya majirani wazipata kupitia kelele za ugomvi huo zilizokuwa zikirindima pande hizo, kwani kwa wakati huyo marehemu Kanumba alikuwa akioga kujiandaa kutoka, Lakini kama imeshaandikwa na Sir God ujue imefika tu, na ndipo aliposukumwa na mpenziwe huyo kwa kukwepa asinyang'anywe simu na kubaini janja yake.
 
Eti ndipo alipoanguka na akafikia kichwa na hivyo akapoteza fahamu, huku mpenziwe huyo akihisi anataniwa kama wawapo katika 'SINI' ya maigizo, lakini kila alipojaribu kumsemesha na kumuamsha hakuona dalili ndipo alipoamua kumtwangia simu daktari mmoja ili afike kuokoa jahazi mahala hapo.
 
Mbali na daktari huyo pia walifika wakali kibao pande hizo, mdogo wake pamoa na mjsanii mwenzake, Vicent Kigosi 'Ray' ambaye alipohojiwa na moja ya kituo cha Redio ya jijini, alisema kuwa baada ya kufika mahala hapo na kujaribu kila jitihada za kumuamsha hazikuzaa matunda na ndipo walipogundua kuwa mkali huyo alikwishapoteza uhai wake.
 
Aidha Afande Kenyela alisema kuwa alipigiwa simu na ndugu wa Kanumba ambaye walikuwa wakiishi pamoja na Kanumba na walipofika eneo la tukio  walikuta tayari ameshakata roho ila bado inasubiriwa ripoti ya daktari.

Kamanda Kenyela, aliendelea na kusema kuwa mpenzi wake Maerehemu Kanumba, aliyetambulika kwa jina la Lulu,  hivi sasa anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi.
 
Lulu ambaye naye anag’aa kwenye tasnia ya Filamu amekuwa akigonga vichwa vya habari vya magazeti ya “udaku” kutokana na skendo za mara kwa mara za mahusiano ya kimapenzi na wakali mbalimbali, ambapo ni majuzi tu mwanadada huyu ametimiza miaka 18 tangu kuzaliwa.

Aidha nyumbani kwa marehemu Sinza kumejaa ndugu jamaa na marafiki kiasi barabara ya kwenda Lion kupitia Madukani inapitika kwa taabu.

Kanumba ambaye alizaliwa mwaka 1984 amefanikiwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya movie za Tanzania si tu kwa Tanzania bali hata nje ya mipaka ya nchi pia.

Kwa mashabiki wa filamu za kibongo Kanumba alikuwa ni namba moja na kwa kiasi kikubwa aliweza kuweka viwango kwani alikuwa anafaa kwa kila kona kuanzia kuigiza mpaka kuvaa na adamu ya maisha tofauti na ma Super Star wengine hivyo kuwavutia watu wa rika lote.
 
 Kanumba anamaliza kipindi chake cha miaka 28 akiwa ameacha kumbukumbu ambayo itaishi kwa muda mrefu.

Kanumba anatarajia kuagwa siku ya Jumanne katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE, AMEN

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.