Habari za Punde

*AMOS MAKALA ATUA KINYENZE MVOMELO KUTATUA MGOGORO WA ARDHI

 Mzee Said Ahamad Kondo ( aliyesimama) akiuliza maswali  kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Mvomero , Amos Makalla ( hayupo pichani) alipokuwa katika  Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali kufuatilia mgogoro kati ya Wananchi hao na Mwekezaji wa Kizungu.
 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( aliyesimama) akisisitiza jambo juu ya namna ya kutafuta muakafa ili  kumaliza  mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kitongoji cha Kinyenzi dhidi ya Mwekezaji wa kizungu.
 Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Jafari ( aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa  mgogoro wa shamba namba 296  kati  ya wanachi wa Kitongoji cha Kinyenze na Mwekezaji wa Kizungu wakati wa  mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo , uliofanyika hivi karibini wenye lengo  la  utatuzi wa mgogoro huo.
Baadhi ya wazee na wananchi wa Kitogoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera,Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo hilo, Amos Makalla ( hayupo pichani) wakati alipowatembelea hivi karibuni, wananchi wa Kitongoji hicho kwa ajili ya kupanga mkakati wa kumaliza mgogoro kati ya mwekezaji wa kizungu na wakazi hao, Mbunge huyo pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo. Picha kwa Hisani ya FATHER KIDEVU 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.