Zitto Kabwe, Mb.
Benki Kuu ya Taifa lolote ndio taasisi pekee yenye takwimu zote nyeti na za uhakika zinazohusu uchumi wa Taifa hilo. Katika tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania eneo la Machapisho kuna Taarifa nyeti sana mbili, Mapitio ya Uchumi ya Mwezi (Monthly Economic Review) inayotoka kila Mwezi katika Mwaka na Mapitio ya Uchumi ya Robo Mwaka (Quarterly Economic Bulletin). Taarifa hizi hutoa taarifa kuhusu masuala yote muhimu yanayohusu Uchumi wa Jamhuri ya Muungano na Uchumi wa Zanzibar ikiwemo taarifa za Mfumuko wa Bei, Mapato na Matumizi ya Serikali, Mwenendo wa Biashara ya Kimataifa na Deni la Taifa.
Ukienda kwenye tovuti ya Benki Kuu leo utakuta Taarifa hizi. Lakini Taarifa hizi zimeishia Desemba mwaka 2011 zikitaarifu masuala ya Uchumi ya Mwezi Novemba na robo ya mwaka inayoishia Desemba. Ukitaka kujua Bajeti ya Serikali na mwenendo wake hutapata taarifa za sasa bali za Mwezi Novemba mwaka 2011, miezi sita nyuma. Huu sio utendaji uliotukuka. Hii ni kuficha taarifa kwa wananchi. Taarifa zinafichwa ili iwe nini? Nani anafaidika na kufichwa kwa taarifa muhimu kama hizi?
Kuna tetesi kwamba Hazina ya Taifa (Hifadhi ya Fedha za kigeni – foreign reserve) inakauka, kwamba tuna hifadhi ya kuagiza bidhaa nje kwa mwezi mmoja tu. Niliposikia tetesi hizi sikuamini. Nilipoenda katika tovuti ya Benki Kuu ili kuweza kuwa na habari rasmi (authoritative) nimekuta takwimu za Novemba 2011.
Takwimu ya Mfumuko wa Bei iliyoko kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania ni ya mwezi Novemba mwaka 2011!
Ukitaka kujua mwenendo wa Bajeti ya Serikali kama makusanyo ya Kodi na Matumizi utapata Taarifa ya Mwezi Novemba mwaka 2011.
Ukitaka kujua manunuzi ya Mafuta (fuel imports) kwa miezi 3 ya mwanzo ya mwaka 2012 ili kuweza kuona namna Umeme wa dharura umeathiri urari wetu wa Biashara ya Nje hupati taarifa hiyo katika tovuti ya Benki Kuu.
Taarifa zinafichwa.
Ndio. Zinafichwa tena makusudi maana taarifa hizi zipo Benki Kuu. Huu ni uzembe maana Nchi inawalipa wafanyakazi wa Benki Kuu mishahara minono ili wafanye kazi hizi. Benki Kuu pia imetoa zabuni kwa Kampuni Binafsi kuchapisha Taarifa hizi. Kama Taarifa hazitoki kwa wakati ni wizi. Wizi ambao haupaswi kufumbiwa macho.
Benki Kuu ya Tanzania ipo miezi Sita nyuma. Aibu kubwa sana.
Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano akihakikishia mataifa duniani kuhusu uwazi Serikalini (#OGP), Taasisi kubwa kama Benki Kuu inaficha Taarifa ambazo ni nyeti kwa wananchi na muhimu kwa wafuatiliaji wa sera za Serikali. Rais wa nchi anaongea Buluu, Gavana wa Benki Kuu anasimamia Kijani!
Inaudhi na kukera sana kwenda kwenye tovuti ya Benki Kuu na kukuta taarifa za miezi Sita iliyopita. Benki Kuu hamstahili kuitwa Benki Kuu, labda benki kuu kuu. Rekebisheni jambo hili haraka sana maana kuficha taarifa kwa Umma ni ufisadi. Haki ya kupata taarifa ni haki ya msingi katika Katiba yetu. Hatutaki kushtukizwa na kuambiwa Hazina ya Taifa imekauka.
Prof. Ndulu hakikisha Taarifa ya Mapitio ya Uchumi wa kila Mwezi imewekwa kwenye tovuti kwa muda mwafaka. Ifikapo mwisho wa Wiki inayoanzia Jumatatu Mei 14, tovuti ya Benki Kuu iwe na Taarifa za miezi yote (Desemba, Januari, Februari, Machi na Aprili). Taarifa hizi ni muhimu ili nasi tutekeleze majukumu yetu ya Kikatiba kama Wabunge, Mawaziri vivuli na Wananchi wa Tanzania.
|
*BENKI KUU: HAZINA YA TAIFA IMEKAUKA???
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MATANGAZO MADOGO MADOGO
MAFOTO PRODUCTION & ENTERTAINMENT KWA MAHITAJI YAKO YA STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING, MUSIC & Mc's KATIKA SHEREHE YA AINA YEYOTE. VIDEO EDDITING, COVER DISGNING, PPS ZA DK 3, POSTERS ZA AINA MBALIMBALI COVER CD PRINTING, BURNING CD N.K. WASILIANA NASI KWA NO, 0787 200005/0754, 0655-306109/0714 656660 BARUA PEPE:- muhidinuk@yahoo.co.uk,sufianimafotoblog@gmail.com AMA TEMBELEA www.sufianimafoto.com
BLOGU RAFIKI
-
-
MEXICO YAANZA VYEMA KOMBE LA DUNIA, YAICHAPA AFRIKA KUSINI 2-0 - WENYEJI, Mexico wameanza vyema Fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya ushindi wa mabao 2–0 dhidi ya Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi A usiku wa kuam...13 hours ago
-
SERIKALI YATOA FEDHA KUJENGA SHULE MPYA YA SEKONDARI KATA YA MSANJA, KILINDI. - Wananchi wa Jimbo la Kilindi wamepokea kwa furaha taarifa ya Serikali kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Kata ya Msanja, K...1 day ago
-
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA SLOVAKIA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI - Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Ulaya wa Jamhuri ya Slovakia, Mhe. Juraj Blanár, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi kuanzia Juni 10 hadi 11, 2026,...1 day ago
-
Rais Mstaafu Dkt. Kikwete Akutana na Rais wa Kenya wakati wa mkutano wa Jukwaa la Amani la Oslo 2026 - Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. William Samoei Ruto walipokutana wakati wa mkutano wa Jukwaa la Amani la Osl...1 day ago
-
MAKALA :Uchumi wa Nyuklia: Uchambuzi wa akiba ya urani ya Mkuju na maono ya Rais Samia ya kinu cha kwanza mwaka 2029 - *Na Beda Msimbe, TBN, aliyekuwa Urusi* Kwa miaka mingi, mazungumzo kuhusu nishati nchini Tanzania yamekuwa yakitawaliwa na vyanzo vya maji, gesi asil...2 days ago
-
MAFUNZO KWA WAFANYAKAZI WA TCAA YAWEKA MKAZO KATIKA UTENDAJI, USHIRIKISHWAJI WA WADAU NA MAENDELEO YA SEKTA YA ANGA - Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dkt. Jabiri K. Bakari, amewataka watumishi wa Mamlaka hiyo kuendana na mabadiliko kwa kujen...2 days ago
-
TANZANIA NA MAREKANI ZASONGA MBELE KUKAMILISHA MAKUBALIANO MAKUBWA YA UWEKEZAJI - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Andrew L...6 months ago
-
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini ke...1 year ago
-
-
BODI YA MAJI BONDE LA KATI YAWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI KUFUATIA MAFURIKO KWENYE MAZIWA YA KINDAI, MUNANG NA SINGIDANI - * Mhandisi Rasilimali za Maji, Bodi ya Maji Bonde la Kati, Moses Salumbi (kushoto), akiweka alama za ukomo wa maji ya mafuriko kwenye Maziwa ya Kindai na...6 years ago
-
MSANII DIAMOND AZINDUA WIMBO WA COLOURS KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI - Cathbert Kajuna To:amichuzi,othmanmichuzi,MUHIDIN MICHUZI,Geofrey Adroph Bcc:fungoomar@yahoo.com May 15 at 6:00 AM Msanii Diamond akipagawisha mashabiki wa...8 years ago
-
RAIS JOHN MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA JCA NA BALOZI WA JAPAN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM - *Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shini...8 years ago
-
JOSE MOURINHO HAS REPORTEDLY 'SHOKED' SOME OF HIS MANCHESTER UNITED PLAYERS - *Jose Mourinho might have hoped for a longer honeymoon at Manchester United, but three defeats in a row, in the space of a week, have led to the first maj...9 years ago
-
TIBA YA MAGONJWA YAKO NA MATATIZO MBALIMBALI SASA HII HAPA BEI NAFUU SOMA HAPA KWA MAKINI - Je? Unaumwa au unasumbuliwa na matatizo yoyote kiafya? Unahitaji msaada wa haraka, tuna virutubisho sahihi kuondoa magonjwa kama kisukari, presha, uvimb...9 years ago
-
DIAMOND PLATINUMZ HOUSE 'STATE HOUSE' - Bila shaka muziki unalipa na ndio maana mwanamuziki wa Bongo Fleva, kutoka Tanzania Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz, ameweza kujenga nyumba jambo ambal...11 years ago
-
SIMBA ILIPOWASHANGAZA MASHABIKI WA SOKA JANA,ILIPOCHOMOA MABAO 3 NA KULAZIMISHA SARE YA 3-3 - * Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akiwania mpira na kipa wa Simba Abel Dhaira, wakati wa kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanza...12 years ago
-
-
-
-
No comments:
Post a Comment