Meneja Masoko wa CFAO Motors, Alfred Minja akiwavisha medali baadhi ya washindi wa shindano la kuogelea lililofanyika katika Shule ya Hopac iliyopo jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya Mashabiki wa mchezo wa kuogelea waliohudhuria mashindano hayo.
Baadhi ya washiriki wa shindano la kuogelea wakichumpa kwenye maji.
Baadhi ya washiriki wa shindano la kuogelea wakichumpa kwenye maji.
Na.Mwandishi wetu
Kampuni na taasisi mbalimbali nchini Tanzania zimepewa wito wa kusaidia udhami wa kusaidia mashindano yajayo ya kuogelea ili washiri waweze kuwakilisha vyema na kuitangaza Tanzania.
Amesema mwaka huu mashindano hayo yameonyesha mafikio makubwa kwa kuwa mara ya mwisho kulikuwa na washiriki 170 pekee, lakini sasa wamepata washiriki kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha, Mwanga, Moshi, Morogoro, Zanzibar na dare s Salaam.
Aidha Bw. Ngalinoma ametoa shukrani za dhati kwa kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa magari ya NISSAN ya CFAO Motors kwa kutoa udhamini ikiwa ni pamoja na kuhahakisha mchezo huo unakuwa hapa nchini.
Amefafanua kuwa Mashishindano hayo ni kwa Arika nzima na yatakayoshirikisha vijana na pia kutakuwa na mashindayo ya wazi (Open Chmpionship) yatakayofanyika kuanzia mwezi Septemba tehe Mosi na terehe 2.
Vilevile amesema wakati huo huo watakuwa wanamuandaa mwogeleaji mmoja anaitwa Magdalena Moshi anayekwenda kushiriki michuano ya Olimpiki ikiwa ni pamoja na kufanya mafunzo mikoani ili kuhakikisha mchezo huo unaendelea nchi nzima.
Akizungumza Mkurugenzi wa Masoko wa CFAO Motors Bw. Alfred Minja amesema kampuni hiyo inakusudia kufanya mazungumzo na chama hicho na kuangalia njia watakazo tumia kuwalea na kuwaendeleza wachezaji wa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment