Habari za Punde

*HAYA NI MAAMUZI YA HALMASHAU YA MJI WA DODOMA AU NI MTU BINAFSI?

 Pamoja na kuwapo kwa malalamiko mbalimbali ya kuuzwa kwa maeneo mbalimbali yasiyostahili kwa wawekezaji na wafanyabiashara ambayo hutumika kwa matumizi tofauti na mahala husika, lakini bado inaonekana maagizo haya yanazidi kupuuzwa. 

Lakini hadi mmiliki wa jengo hili lililopo Mtaa wa Majengo mjini Dodoma, anaanza kujenga hadi kukamilka na kufikia hatua hii, wahusika hawajaona tofauti na matumizi  ya jengo hili na barabara hii ambayo ina mzunguko 'Round About' jambo ambalo linaweza kusababisha ajali zisizotarajiwa kutokana na dereva kutoona kinachotokea upande wa pili kwa jengo hilo kuzidi na kuingia barabarani.
Gari likipita mbele ya jengo hilo baada ya kuzunguka 'Round About' huku dereva akiwa haoni anakotakiwa kwenda kutokana na jengo hili kujengwa kinyume na utaratibu. Baadhi ya madereva wa daladala wa mjini Dodoma waliochonga na Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, walisema kuwa wengi wao wamekuwa wakipata tabu wafikapo eneo hilo na hasa gari linalokuwa likitoka eneo la Soko la Majengo kueleke Tamisemi. 
JE WAHUSIKA MLIFIKIRI MARA MBILI KABLA YA KUTOA MAAMUZI YA KUJENGWA JENGO HILI?

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.