Habari za Punde

*MAKAMPUNI 14 YAJITOKEZA KUDHAMINI REDD'S MISS KURASINI 2012

Miss Kurasini anaeshikilia taji ambaye pia ni Top Model wa Miss Tanzania 2011, Mwajabu Juma.

JUMLA ya wadau 14, wamejitokeza kudhamini ili kufanikisha shindano la Redd's Miss Kurasini 2012, ambalo linataraji kufanyika Mei 25 mwaka huu katika ukumbi wa Equator Grill.

Akizungumza na Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Mkurugenzi wa ZUM Fashion & Entertainment, Zuwena Mustapha,  alisema kuwa mbali na Kampuni ya Bia Tanzania kudhamini shindano hilo kupitia kinywaji chake cha Redds, pia makampuni kadhaa yamevutiwa na kujitokeza  kudhamini shindano hilo.

“Napenda kuwatangazieni kuwa hadi sasa shindano letu la Miss Kurasini yameshajitokeza jumla ya makampuni 14 kudhamini shindano letu, lakini bado milango ipo wazi kwa yeyote anayependa kutudhamnini na kusaidia warembo wetu wa kurasini kupata zawadi nono na shindano kuwa zuri,”alisema Mustapha.

Aliwataja wadhamini wakuu wa shindano hilo ni Nameems Wear wakisaidiwa na Reds, Dodoma wine, Clouds FM, Lady Pepeta, Father Kidevu Blog, Jambo Leo, Aucland Tours & Safaris, Candy Bureau de Change, Flexip, PJ Amusement, Renzo Salon na Madishisha Video Production.

Aidha Jumla ya warembo 16 wamejitokeza kuwania taji la Redds Miss kurasini 2012, ambalo taji linashikiliwa na Top Model wa Miss Tanzania 2011, Mwajabu Juma.

Akiwataja warembo waliopo kambini na kunolewa na Mwajabu Juma akisaidiwa na Malkia wa vipaji wa Miss Tanzania 2011, Rose Hurbert ni Mariam Sadic (19), Johari Juma (20),Linda Deus (20),Irene Sostheness 20),Neemadoree Sylvery(29),Edna Magige (22), Lindanancy Joseph(20), Elizabeth Mkende (19), Betty Peter (22), Jennifer Njabili (18), Lilian Joseph (20), Farida Mrope (23),Christina Moses (20), Angle Gasper (19), Flaviana Maeda(22) na Sia Kimambo (19).

Shindano hilo la Urembo ya Miss Tanzania katika kituo cha Kurasini yanategemea kupambwa na burudani kali kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao watatangazwa hivi karibuni.  

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.