Habari za Punde

*MASAWE MTATA KUTAMBULISHA WIMBO WAKE MPYA KATIKA PAMBANO LA NGUMI LA UBINGWA WA TAIFA KINONDONI VIJANA HALL LEO

Masawe Mtata, akiwa katika Studio za Magic Star, akimalizia wimbo wake wa Uongo Kweli, ambao atautambulisha leo hii kwa mara ya kwanza.
 MSANII wa vichekesho anayeigiza na kundi lake la Ze Commedy linalorusha michezo yake kupitia Televisheni ya Chanel 5, Masawe Mtata 'Kicheko', leo anatarajia kupanda jukwaani kutambulisha wimbo wake mpya uendao kwa jina la Uongo Kweli.

Masawe, atatambulisha wimbo huo katika pambano la Ngumi la Ubingwa wa Taifa (TPBO) kati ya james Mokiwa kutoka Kinondoni na Ramadhan Kumbele kutoka TMK, litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Vijana Konondoni, ambapo mgeni rasmi katika pambano hilo atakuwa ni Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan.

Wimbo huo wa Masawe, ni miongoni mwa nyimbo zake nane zitakazokamilisha albam yake anayoendelea kurekodi katika Studio za Magic Star zilizopo Sinza White Inn, chini ya mwandaaji, Sebastian Mhina 'Criston' na kufanyiwa mixing na Abraham Kazi 'Adda X'.

Aidha Pambano hilo la ngumi leo pia litasindikizwa na burudani nyingine kutoka kwa Mkali wa Hip Hop, Kala Pina na msanii wa muziki wa Bongo Flava, kutoka Singida, Chuang.
Mwandaaji, Sebastian Mhina 'Criston', akielekezana jambo na Masawe Mtata, wakati wakifanya mixing ya wimbo hio wa Uongo Kweli.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.