" SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI"
Bendi ya maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" (FFU) yenye maskani yake nchini Ujerumani, imetuma salamu za hongera na pongezi nyingi kwa wanahabari na vyombo vya habari vyote duniani, katika sherehe ya siku ya "uhuru wa vyombo vya habari"
Bendi hiyo inawapongeza wanahabari na vyombo vyao, kwa kazi muhimu wanazofanya za kuwapasha habari walimwengu Duniani kote, kwani mchango wa wanahabari katika jamii duniani, ni sawa na mbolea katika maisha ya kila siku, kwani maisha bila ya habari, ni sawa miti bila mizizi.
Hongereni sana wanahabari na Wanalibeneke wote duniani.
FFU wa Ngoma Africa band sasa wanatamba na Song lao jipya "Uhuru wa habari" wimbo ambao unasikika ama unaweza kuusikia au kuupata kupitia www.ngoma-africa.com
au http://www.ngoma-Africa.com
No comments:
Post a Comment