Ulimwengu, mfungaji wa bao la Ngorongoro |
Katika mchezo wake wa jana usiku, Ngorongoro
imekubali kipigo cha mabao 2-1 ugenini, kwenye Uwanja wa Khartoum,
baada ya awali kushinda 3-1 Uwanja nyumbani wa Taifa, Dar es Salaam wiki mbili zilizopita
na sasa itachuana na Nigeria Raundi ya Pili, mechi ya kwanza ikicheza Julai 28,
mwaka huu Dar es Salaam.
Sudan
walipata mabao yao kupitia kwa Mohammed Abdelrahman, katika dakika ya 10 na Ahmad Nasr
kwa penalti dakika ya 65, wakati bao la Ngorongoro lilifungwa na mshambuliaji wa
TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu kabla ya mapumziko.
Ngorongoro
Heroes wanatarajia kurejea nchini leo Jumapili majira ya Saa 3
asubuhi.
Mshindi
kati ya Ngorongoro na Nigeria atamenyana na mshindi kati ya Afrika Kusini na
Kongo Brazzaville, mechi ya kwanza ikichezwa kati ya Septemba 21 na 23 mwaka huu
ugenini na marudiano Oktoba 6.
No comments:
Post a Comment