Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Lindi wakati wa maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi jana. Mhe Spika alikuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele hicho.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akipokea DVD maalumu kuhusu Albino na Maisha yao kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Under the Same Sun Bi. Vicky Mtetema wakati wa maadhimisho ya Siku ya Albino yaliyofanyika Lindi. Shirika hilo ni mdau mkubwa wa watu wenye ulemavu wa Ngozi na linajishughulisha na kutoa elimu kwa watu wenye Ulemavu wa Ngozi pamoja na Misaada mbalimbali. Spika walikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi Jana.
Mhe. Spika akioneshwa mojawapo ya mafuta maalumu ya kuzuia Mionzi ya Jua ambayo hutolewa bure na Serikali kupitia taasisi ya magonjwa ya Ngozi kwa watu wenye ulemavu wa Ngozi.
No comments:
Post a Comment