Wanafunzi wa Darasa la Kwanza katika Shule ya Msingi Makumbusho, iliyopo Jijini Dar es Salaam, kama walivyonaswa na kamera ya Sufianimafoto wakiwa wamekaa chini wakati wakisubiri mwalimu kuendelea na Vipindi.
Wazazi wengi wamekuwa wakilalamikia elimu duni ambayo huenda ikawa ikisababishwa na na mambo kama haya, ambapo Mzazi analazimika kumlipia mwanawe Nauli ya kila siku kwenda na kurudi shuleni pamoja na hela ya kutumia shuleni, Hela ya Twisheni na 'Buku' 1000 kwa ajili ya mtihani wa kila mwezi hela ya uji Ndoo ya maji, Fagio, Jembe, Reki, Hela ya mafunzo ya Kompyuta, na mengineyo, lakini bado mzazi anashuhudia mtoto wake akisoma katika mazingira kama haya Je Ungelikuwa wewe ndo unamwona mtoto wako katika hali hii Michango hiyo ingesomeka??
No comments:
Post a Comment