Askari wa Hospitali ya Muhimbili, wakimuokoa mwananchi aliyenusurika kwa kipondo cha aja kutoka kwa Madaktari waliomshuku kuwa jamaa huyu ni mmoja kati ya watu wa usalama wakati akikatiza anga hizo walipokuwa katika harakati za kumsaidia kiongozi wao, ambapo walimvamia na kuanza kumshambulia kabla ya kuokolewa na askari hao.
Hata hivyo Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova, akizungumza na waandishi wa habari jana alionya juu ya wananchi kuchukua sheria mikononi bila kufuata sheria kwa kuwa zinaweza kuleta madhara hata kwa ndugu zao kwani kachelo huyo alikuwa kazini na ndiye aliyefanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa suala la Dk. Steven Ulimboka linashughulikiwa vizuri ikiwa ni pamoja na kuletwa hospitalini hapo. Picha na Full Shangwe
No comments:
Post a Comment