Habari za Punde

*COPA CABANA BEACH RIO JANEIRO-BRAZIL

 Kijana Msanii wa michoro na msanifu, akiwa pembeni ya 'Picha' ya moja na kivutio cha Utalii ya Jijini Janeiro Brazil, aliyoijenga kwa kutumia mchanga pembezoni mwa Ufukwe wa Copa Cabana, ambapo kila anayehitaji kupiga picha mchoro huu analipia kiasi chochote atakachojisikia 'Changia Chochote', ambapo siku za kawaida kijana huyu huweza kukusanya kiasi cha Real 20, 000/= na zaidi na siku za sikukuu ama msimu wa Watalii hukusanya kiasi kikubwa cha peasa yao 'Real'. Pembezoni mwa Ufukwe huu wapo vijana wengi tu ambao hufanya shughuli hii kwa kujenga michoro tofauti tofauti inayoonyesha mji wa Rio.
 Sehemu ya eneo la Ufukwe huo wa Copa Cabana na Mandhari nzuiri inayovutia kwa usafi. Eneo hili ambalo huwavutia wageni wengi wanaoingia mji wa Rio, hufanyiwa usafi kuanzia usiku wa saa tano ambapo magari ya usafi kupita na kuokota taka zote.
Sufianimafoto, akinasa kumbukumbu.
 Mandhari inayovutia na kuhamasisha.
 Eneo hili pia kuna kila aina ya michezo, kama ambavyo watu hawa wanaonekana wakifundishana Sarakasi kwa kutembea juu ya Kamba.
Huyu ni mwalimu wa huyu mwanadada, akimuonyesha jinsi ya kufanya baada ya kumfundisha huku kila dakika akianguka bila kumaliza umbali uliowekwa wa kama mita 10.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.