Habari za Punde

*KIM ATAJA KIKOSI CHA KUIVAA IVORY COAST LEO, KILA LA KHERI STARS

 Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa, Kilimanjaro Taifa Stars wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho leo asubihi kujiandaa na mechi yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast  leo katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast. Kikosi hicho kinashuka dimabani leo kukabiliana na Ivory Coast.
 Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Taifa Stars, Kim Poulsen, akizungumza na wachezaji wake baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kujiandaa na mechi  yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast leo katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast.
 Kocha wa Makipa wa Kilimanjaro Taifa Stars, Juma Pondamali, akiwanoa makipa wa timu hiyo ikiwa ni hatua ya mwiso kabla ya kuvaana na Ivory Coast leo kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast.

Mshambuliaji  Kilimanjaro Taifa Stars, Mbwana Samatta, akiweka saini kwenye madaftari ya vijana wa Ivory Coast  baada ya kumaliza  mazoezi ya kujiandaa na mechi yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast. Samatta amekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wengi wa Ivory Coast.
*********************************************
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen, ametaja kikosi cha cha kwanza kitakachoanza kuivaa Ivory Coast leo  katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, katika mechi yake ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia.
 
Kima amefanya mabadiliko katika nafasi mbili ya kikosi kilichocheza mechi ya kimataiafa ya kirafiki Mei 26 mwaka huu ya kujipima nguvu na Malawi (The Flames) iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu.
 
Amir Maftah atacheza beki wa kushoto badala ya Waziri Salum wakati Mrisho Ngasa atakuwa mmoja kati ya washambuliaji wa mwisho. 

Ngasa atacheza nafasi ya Haruna Moshi ambaye hayuko na Stars nchini Abidjan baada ya kuumia wakati akiwa mazoezini siku moja kabla ya safari.
 
Kikosi kamili cha Taifa Stars ambayo itatumia mfumo wa 4-4-2 ni kima ifuatavyo;
 
Kipa; Juma Kaseja
 
Mabeki; Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris na Kevin Yondani
 
Viungo; Shabani Nditi, Salum Abubakari, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto
 
Washambuliaji; Mbwana Samata na Mrisho Ngasa
 
Wachezaji wa akiba; Mwadini Ali, Waziri Salum, Juma Nyoso, Erasto Nyoni, John Bocco, Simon Msuva, Jonas Mkude, Christopher Edward na Ramadhan Singano.
 
Kim amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na kilichobaki ni kwa wachezaji kudhibitisha maandalizi hayo kwenye dakika 90 za mchezo huo utakaoanza saa 11 kamili jioni (nyumbani itakuwa saa 2 kamili usiku).
Mechi hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia televisheni ya RTI ambapo itaonekana katika nchi 58 duniani.
 
Mwamuzi; Slim Jedidi (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba 1; Bechir Hassani (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba mbili; Sherif Hassan (Misri)
Mwamuzi wa akiba; Youssef Essrayri (Tunisia)
 
Mtathmini wa waamuzi; Rachid Medjiba (Algeria)
Kamishna wa mchezo; Saleh Issa Mahamat (Chad)
 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
+22504456347
Abidjan

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.