PICHANI: ni Dkt. Ulimboka, akiwa katika hali mbaya akiwa amevimbiana uso na mdomo baada ya kuokotwa akiwa hoi hajitambui, katika Msitu wa Mabwe Pande, leo asubuhi.
Ulimboka, alitekwa jana mida ya saa 6 usiku baada ya kupigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Abeid na alitekwa na watu wawili waliokuwa na silaha.
Habari zinasema kuwa baada ya kutokea kwa tukio hili la kutekwa kwa Kiongozi huyu wa Madaktari, aliyekuwa akiongoza mgomo huo sasa imeelezwa kuwa hali imezidi kuwa mbaya zaidi Hospitalinihapo ambapo kwa sasa na wafanyakazi wa chumba cha maiti Muhimbili nao wamegoma kufanya kazi na mgomo huenda ukawa mkubwa zaidi, Aidha imeelezwa kuwa Madaktari hao walio katika mgomo wamekuwa wakihaha huku na huko kumtibia kiongozi wao na hali ya vurugu imeipotia hospitalini hapo ambapo tayari mtu mmoja ameripotiwa kujeruhiwa na madaktari hao baada ya kumuona akikatiza maeneo hayo huku akiwa amevalia Kaunda Suti, na kumvamia na kuanza kumshambulia wakimhisi kuwa ni mmoja kati ya askari wa Usalama. MLIOVALIA SUTI AU KAUNDA SUTI LEO SI SIKU NZUZI KUKATIZA MITAA YA MUHIMBILI. Picha kwa Hisani ya Jamiiforums
No comments:
Post a Comment