Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Italy, Mario Balotelli (kulia) akishangilia na kucheka baada kufunga bao wakati wa mchezo wa nusu Fainali wa kuwania Kombe la Euro 2012, kati ya timu yake na Ujerumani, uliochezwa jana usiku.
Italy waliibuka washindi kwa mabao 2-1, huku mabao yote yakitiwa kimiani na Balotelli, katika dakika ya 20 na 36 katika kipindi cha kwana, huku bao la kufutia machozi la Ujerumani likifungwa na Mesut Oezi, kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 91.
Kwa ushindi huo sasa Italy watashuka dimbani siku ya Jumapili kuwavaa Spain katika Fainali, baada ya Spain nao kuwaondoa Ureno kwa mikwaju ya penati 4-2 juzi usiku.
Kipa wa Ujerumani, Manuel Neue, akijaribu kuilazimisha Nyonga kurudi upande wa pili ili kuokoa shuti la Mshambuliaji wa Italy, Mario Balotelli (katikati) bila mafanikio, wakati wa mchezo huo uliochezwa jana usiku.
Mashabiki wa Italy, wakishangilia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ujerumani, baada ya kumalizika kwa mchezo huo jana.
Baada ya mchezo huo Jiji zima lililipuka kwa shangwe na nderemo ambapo ilikuwa ni furaha kwa mashabiki wa Italy na kilio kwa mashabiki wa Ujerumani.
Mashabiki wa Ujerumani waliokuwa wakifuatilia mchezo huo kupitia Screen nje ya uwanja huo wakiwa hawaamini kinachotokea ndani ya uwanja huo.
Shabiki huyu wa Ujerumani akiwa haamini kilichoitokea timu yake baada ya kupigwa bao 2-1 na mpira kumalizika, ambapo alijikuta akiwa amebakia peke yake uwanjani hapo huku akiwa amejifunika uso asione kinachoendelea, wakati mashabiki na wachezaji wa Italy wakishangilia ushindi wao.
Mashabiki hawa wa Ujerumani pia walikuwa makini kufuatilia mchezo huo kupitia Screen katika maeneo ya jiji hilo, lakini nao wakiwa hawaamini kinachotokea uwanjani.
No comments:
Post a Comment