Habari za Punde

*MAOFISA HABARI NA MAWASILIANO WA SERIKALI WATEMBELEA HIFADHI YA SERENGETI

 Baadhi ya maofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili kwenye lango la kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  mkoani Mara ikiwa ni moja ya mkakati wa kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
 Maofisa habari wakipata kifungua kinywa katika  eneo la Lamadi lililopo mkoa mpya wa Simiyu wakiwa njiani kuelekea katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.
 Mfanyabiashara wa supu katika eneo la Lamadi mkoani Simiyu Bw. Sobia Majuto akiwahudumia baadhi ya wateja wake ambao ni maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali walipokua njiani kuelekea katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti .
 Wanyama aina ya Twiga ambao ni moja ya kivutio kikubwa  katika hifadhi ya taifa ya Serengeti wakitembea kwa mstari ndani ya hifadhi hiyo.
 Kundi kubwa la Nyumbu, wakiwa katikati ya Barabara ndani ya hifadhi hiyo na kuufanya msafara wa magari yaliyokuwa maofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali kwenda kwa mwendo wa polepole, Kwa mujibu wa taratibu za hifadhi ni kosa kwa dereva  kupiga honi, kuendesha gari kwa mwendo kasi au kupiga honi ndani ya eneo la hifadhi.

 Mnyama aina ya Simba maarufu kwa jina la mfalme wa mwitu akipanda mti ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti  na kuwafanya maofisa Habari na Mawasiliano wa serikali kushangaa uwezo wa Simba huyo. Simba wa aina hii wanaoishi ama kupanda juu ya miti hupatikana ndani ya Hifadhi ya Serengeti pekee. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.